Stadi ya SMILE inahusu nini?

Stadi ya SMILE ni stadi yautafiti unaohusu kujielimisha kuhusu matukio ya Maisha(ikiwa pamoja na  changamoto na ustawi wa jumla) wa watu wanaojitambulisha kama wa jinsia/kijinsia ya walio wachachi(SGM). Inafanyika katika nchi tatu: Brazil,Kenya na Vietnam. Jinsia au kijinsia ya walio wachache inaweza maanisha watu ambao ni LGBTQI (wasagaji,mashoga,wanaoshiriki ngono na jinsia mbili tofauti, wenye jinsia tofauti na waliozaliwa nayo,wasiofuata mtindo wa kingono wa kawaida au waliozaliwa na jinsia mbili tofauti) jinsia au kijinsia ya walio wachache yaweza pia maanisha watu wanaovutiwa na jinsia/ kijinsia ilio sawa na yao, au watu ambao wanajihisi kuwa si wa jinsia/kijinsia waliopewa wakati wa kuzaliwa, au watu wasiojihisi kuwa wa kiume au wa kike.

Kushiriki katika study haswa inamaanisha kukamilisha hili dodoso la mtandaoni itakayochukua dakika 60-90. Hutafaidika kwa njia yoyote kwa kufanya utafiti wa stadi hii.


Mbona nishiriki katika SMILE, ikiwa sifaidiki moja kwa moja?

Lengo letu ni kukusanya data kutoka kwa wanajamii wengi inavyowezekana wa LGBTQI wanaoishi Brazil, Kenya na Vietnam, ili kunakili changamoto nyingi zinazowakabili wanaSGM na kuelewa jinsi sera, mipango na huduma yanavyoweza undwa au badilishwa ili kusaidia na kutoa usaidizi  kwa wenye jinsia au kijinsia ya walio wachache wanoishi katika nchi yako.

Tafadhali saidia jamii yako kwa kuchangia data kuhusu uzoefu wako kama mwenye jinsia au kijinsia ya walio wachache.


Habari yangu italindwa kivipi?

Ili kusaidia kulinda usiri wenu, hatutawai uliza jina lako: hata hivyo, ili kuwasiliana nawe kwa tafiti fuatiliaji tutaulizia nambari ya simu na anwani ya barua pepe, ambayo inahifadhiwa mbali na majibu yako ya utafiti. Habari ya kuwasiliana nawe itaekwa mbali na haitashirikiwa na mtu yeyote asiyehusika na mradi huu.