Stadi inayohusu Afya ya Kiakili na Ustawi kati ya wenye jinsia na kijinsia ya walio wachache nchini Brazil, Kenya na Vietnam

Stadi ya SMILE inahusu nini?

Stadi ya SMILE ni stadi ya utafiti unaohusu kujielimisha kuhusu matukio ya Maisha(ikiwa pamoja na  changamoto na ustawi wa jumla) wa watu wanaojitambulisha kama wa jinsia/kijinsia ya walio wachache (SGM). Inafanyika katika nchi tatu: Brazil,Kenya na Vietnam. Jinsia au kijinsia ya walio wachache inaweza maanisha watu ambao ni LGBTQI(wasagaji,mashoga,wanaoshiriki ngono na jinsia mbili tofauti, wenye jinsia tofauti na waliozaliwa nayo,wasiofuata mtindo wa kingono wa kawaida au waliozaliwa na jinsia mbili tofauti) jinsia au kijinsia ya walio wachache yaweza pia maanisha watu wanaovutiwa na jinsia/ kijinsia ilio sawa na yao, au watu ambao wanajihisi kuwa si wa jinsia/kijinsia waliopewa wakati wa kuzaliwa, au watu wasiojihisi kuwa wa kiume au wa kike.

 

Sisi ni kina nani?

Timu ya utafiti wa SMILE ni ya taaluma nyingi na imebeba watafiti tofauti wenye asili zinazoambatana na wana asili pana ya kufanya kazi mbalimbali katika nchi zenye mapato ya chini na kati na pia kufanya utafiti unaolenga jinsia au kijinsia ya walio wachache (SGMs). Wachunguzi wakuu na wengi wa wanatimu wanajitambulisha kama wenye jinsia/kijinsia ya walio wachache(SGM)

Stadi ya SMILE inafanyika wapi?

BRAZIL

KENYA

VIETNAM

Bado una maswali kuhusu stadi ya SMILE?