Faharasa

Asiyekuwa na jinsia: Mtu asiyejitambulisha na jinsia yoyote. (Agender)

Mshirika: Inamtambulisha yeyote ambaye anaunga mkono kwa uwazi watu wa LGBTQ+. (Ally)

Asiyekuwa na hisia za kimapenzi: Asiyekuwa na mvutio wowote wa kimapenzi na watu wa jinsia lolote. (Asexual)

Anayekuwa na mahusiano na jinsia mbili tofauti: Anayejihusisha kimapenzi au kijinsia na wenye jinsia mbili tofauti na pia mwelekeo wa kijinsia mbili tofauti. (Bisexual)

Cisgender: Mtu ambaye utambulisho wake wa kijinsia unaambatana na jinsia aliyopewa wakati wa kuzaliwa (anajitambulisha kama mwanamke na alipewa jinsia ya kike alipozaliwa AU anajitambulisha kama mwanamme na alipewa jinsia ya kiume alipozaliwa). Kwa kawaida hawafikiriwi kuwa aliyebadilisha jinsia.

Shoga: Mwanamme ambaye ana hisia za kijinsia na kimapenzi kwa/na wanamme wengine. Wanamme na wasio jitambulisha kama mwanamme au mwanamke wanaweza tumia neno hili kujieleza. (Gay)

Uthibitisho wa jinsia: Mchakato ambao unahusisha mpito wa jinsia moja hadi nyingine na unatambulika na kuhalalishwa kwao wenyewe au na wengine. (Gender affirmation)

Utunzi wa uthibitisho wa kijinsia: Inahusu huduma ya afya ambayo inatambua aina mbalimbali za utambulisho wa kijinsia na inasaidia watu kufafanua, kuchunguza na kutimiza utambulisho wa kijinsia (kwa mfano daktari kuitumia jina sahihi alilolichagua mgonjwa au kuagiza tiba ya kubadili homoni kwa mgonjwa mwenye jinsia tofauti na aliyopewa alipozaliwa). (Gender-affirming care)

Upasuaji wa uthibitisho wa kijinsia: Mbinu ambayo mtu mwenye jinsia tofauti na ile aliyopewa wakati wa kuzaliwa anapitia taratibu za upasuaji ili kubadilisha maumbile ya kimwili na/au kazi ya maumbile yao ya sehemu za kisiri ili kufanana na jinsia wanayojitambulisha na kuhusishwa nayo kwa kijumla (kwa mfano upasuaji wa kurekebisha maumbile ya uso, kifua au upasuaji wa "juu", na sehemu za siri upasuaji wa "chini"). (Gender-affirming surgery)

Usemi wa jinsia: Njia ambazo mtu anajieleza na utambulisho wake wa kijinsia (kwa kawaida inahusishwa na kuwa mwanamme au mwanamke) kwa mavazi, majukumu, tabia na kadhalika. (Gender expression)

Utambulisho wa kijinsia: Inamaanisha kujiona kama mwanamme au mwanamke au mchanganyiko wa wote au sio mchanganyiko wa yoyote - jinsi ambavyo watu wanajihisi na kujiita wenyewe. Utambulisho wa kijinsia gfwa mtu unaeza kuwa sawa au utafautiane na jinsia waliopewa wakati wa kuzaliwa. (Gender identity)

Mpito wa kijinsia: Mbinu ambayo mtu anabadilisha maumbile yake ya kiinje ili iambatane kwa karibu sana na utambulisho wake wa kijinsia. Mpito unakaa tofauti kwa kila mtu lakini inaweza husisha kurekebisha chaguo la mavazi, mtindo wa nywele, matumizi ya vipodozi, mitindo ya sauti, tabia na adabu. Kwa wengine, inaweza husisha utaratibu wa matibabu. Sio kila mtu mwenye jinsia tofauti na aliyopewa wakati wa kuzaliwa ana lengo la kupitia mpito na isidhaniwe kuwa mtu angependa kupitia mabadiliko ya kimatibabu. (Gender transition)

Mwenye jinsia sawa: Huyu ni mtu ambaye anavutiwa kimapenzi au kingono na watu wenye jinsia au kijinsia tofauti na yake. (Heterosexual or Straight)

Shoga: Mtu ambaye anavutiwa kimapenzi au kingono na watu wenye jinsia sawa na yake. Wanamme, wanawake na wasiojitambulisha kama wa kiume au wa kike wanaweza kutumia neno hili kujieleza. (Homosexual)

Jinsia tata: Neno la kijumla linalotumika kuwaeleza watu waliozaliwa na sehemu za siri, viungo vya uzazi, na/au mifomu ya kromosomu ambayo haiambatani na ufafanuzi wa kike au kiume. (Intersex)

Msagaji: Mwanamke anayevutiwa kimapenzi au kijinsia na wanawake wengine. Wanawake au wasiojitambulisha kama mme au mke wanaweza tumia neno hili kujieleza. (Lesbian)

LGBTQI+: Ufupi wa msagaji, shoga, anayeshiriki kimapenzi na mwanaumme na mwanamke, aliye na jinsia tofauti na ile aliyopewa alipozaliwa, jinsia mchanganyiko na mengine mengi katika ishara+ ili kutambua mwelekeo wa kijinsia usio na kikomo na utambulisho wa kijinsia unaotumika na wanajamii.

Wanamme wanaovutiwa na wanamme: Hii inamaanisha watu wanaojitambulisha kama wanamme na wanavutiwa kimapenzi au kijinsia na watu wengine wanaojitambulisha kama wanamme. (Men attracted to men)

 Wasiojitambulisha kama wanamme au wanawake: Hii inamaanisha watu wasiojitambulisha kwa kipekee kama mwanamme ama mwanamke. Wanaeza jitambulisha kuwa wote mwanamke au mwanamme au mahali hapo katikati au mahali nje ya hayo makundi mawili ya kijinsia. (Non-binary)

Kujitokeza: Hii inamaanisha mtu ambaye amekubali mwelekeo wake wa kijinsia au utambulisho wake wa jinsia na anashiriki utambulisho huo na wengine. (“Out”)

 Pansexual: Anayejihusisha kimapenzi au kijinsia na wenye jinsia Zaidi ya mbili na pia mwelekeo wa kijinsia wowote (Pansexual)

Jinsia mchanganyiko: Neno linalotumika kwa ujumla kati ya wengi wa watu wenye jinsia au kijinsia ya walio wachache, inajumuisha watu ambao wanajitambulisha kuwa wenye jinsia sawa na/au watu ambao wana vitambulisho vya kijinsia ya wasio jitambulisha kama mme au mke. jinsia mchanganyiko pia inatumika mara nyingi kueleza utambulisho na mwelekeo unaotofautiana na kawaida. hapo awali neno hili lilitumika kama neno la kukera lakini imedaiwa tena na sehemu zingine za harakati ya LGBTQIA+. (Queer)

Kuhoji (utambulisho wa jinsia): Hii inaeleza mtu ambaye anachunguza utambulisho wake wa jinsia. (Questioning - gender identity)

Kuhoji (mwelekeo wa kijinsia): Hii inaeleza mtu ambaye anachunguza mwelekeo wake wa kijinsia. (Questioning - sexual orientation)

Jinsia uliopewa ulipozaliwa: Jinsia (kike, kiume au jinsia tata) ambayo mtaalamu wa matibabu anatumia kueleza mtoto anapozaliwa akizingatia maumbile yake ya nje. (Sex assigned at birth)

Jinsia au kijinsia ya walio wachache: Njia ya ziada ya kueleza jamii ya LGBTQ+ (msagaji, shoga, anayejihusisha na jinsia mbili tofauti, wenye jinsia tofauti na waliozaliwa nayo, jinsia mchanganyiko, na mengine mengi). (Sexual or gender minority people)

Mwelekeo wa kijinsia: Inaeleza vivutio vya kimapenzi na kijinsia wa mtu kwa wengine. (Sexual orientation)

Aliyebadilisha jinsia: Mwenye jinsia tofauti na ile aliyozaliwa nayo. (Transgender)

Mwanamme aliyebadilisha jinsia: Inaeleza mtu anayejitambulisha kama mwanamme na alipewa jinsia ya kike alipozaliwa. (Transgender man)

Mwanamke aliyebadilisha jinsia: Inaeleza mtu anayejitambulisha kama mwanamke na alipewa jinsia ya kiume alipozaliwa. (Transgender woman)

Wanawake wanaovutiwa na wanawake: Inaeleza watu wanaotambuliwa kama wa kike na wanavutiwa kimapenzi au kijinsia na watu wanaojitambulisha kama wa kike. (Women attracted to women)