Utatuzi wa shida za dodoso
Ukurasa wangu wa tovuti uliganda/ kufunga. Nitaweza kurudi aje kwenye dodoso ili kuimalizia?
Ukitumia kifaa kilekile uliotumia kuanza dodoso, bonyeza kiungo cha dodoso la SMILE. Majibu yako ya apo awali yanafaa kuokolewa na unaweza endelea na dodoso.
Ukijaribu kumalizia dodoso lako ukitumia kifaa tofauti, dodoso itachukulia kuwa wewe ni mshiriki tofauti na utapaswa kupeana idhini na kumalizia maswali ya dodoso tena.
Nataka kurudi nyuma na kubadili majibu yangu, lakini dodoso haliniruhusu. Nifanyeje?
Unaweza badili majibu yako katika dodoso ikiwa upo katika sehemu hio kwa kubonyeza kidude la kuruidi nyuma. Hata hivyo, wakati ushasonga mbele kwa sehemu nyingine mpya katika dodoso, unaweza shindwa kurudi nyuma na kubadilisha majibu yako.
Rafiki yangu yuataka kufanya dodoso lakini wakati anapotembelea tovuti inasemekana washafanya dodoso.
Huenda hili ni swala hususi la kifaa. Dodoso linaweza tu kuchukuliwa kutoka kwa tarakilishi ya kipekee/ simu/ kompyuta kibao. Ikiwa watu wawili tofauti watajaribu kufanya dodso kwa wakati tofauti, wakitumia kifaa kimoja(kama simu ya mkononi/ kompyuta ya mkononi inayotumika na watu wote), tovuti itadhani kuwa mtu wa pili ashakamilisha dodoso na hataendelea. Ushauri wetu bora ni kueleza rafiki yako atumie kifaa kingine tofauti(kompyuta ya mkono tofauti au simu tofauti) ili kufikia dodoso.
Napata ujumbe wa makossa katika dodoso, lakini sijui jinsi ya kubadili jibu langu ili dodoso liniwezeshe kuendelea, nifanye vipi?
Tafadhali wasisiliana nasi ukitumia kiungo cha msaada wa kiteknolojia.