Washirika
Ace Africa Kenya ni shirika la kijamii lisilokuwa la serikali inayohusika na kutoa msaada kwa watu walio na maambukizi ya ugonjwa wa HIV/AIDS na makundi iliyo katika hatari kotekatika jamii vijijini nchini Kenya. Ace Africa inafanya kazi katika mchanganyiko wa jamii katika jiji na vijiji, huku ikizingatia haswa maeneo yenye rasilimali duni nchini Kenya na Tanzania. Juhudi zao kuimarisha ujuzi wa wanajamii, , miundo iliopo, washirika wa asasi za kiraia na utawala ili kuongeza uwezo wao na kujitolea kuchukua wajibu wa utunzi na usaidizi kwa wanaoishi na virusi vya HIV na AIDS , watoto na familia yao,mayatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu wametuzwa na ushindi wa 2010 Africa and Middle East wa STARS Foundation Award na STARS Impact Award 2014 ya Ubora katika Utekelezaji wa miradi ya afya ya kijamii.