Kukaa Salama Mtandaoni

Tunakutaka ukae salama ukiwa mtandaoni, ikiwa utashiriki au hautashiriki katika stadi hii. Ikiwa utahifadhi kifaa chako salama, unaweza punguza hatari ya mtu kutazama habari yako ya kibinafsi na uwezekano wa kuitumia habari hiyo kukudhuru. Hapa kuna vidokezo vya kukaa salama mtandaoni:

Programu hasidi na ulinzi wa wadukuzi

Wadukuzi wanaeza shambulia kompyuta yako na kuiba habari yako. Hakikisha kuwa umesakinisha programu itakayokulinda kutokana na virusi, na kuwasha kizingiti ambacho kitazuia mtandao wako kutokana na mitandao nyingine isiyoaminika na pia usiwahi fungua kiambatisho cha barua pepe kutoka kwa watu ambao huwajui na huwaamini. Ikiwa simu yako ama kompyuta yanatenda ajabu, betri inaisha haraka kuliko kawaida na pia inakuwa joto zaidi, mtu anaweza kuwa anafuatilia kifaa chako. Ikiwa wataka kujua zaidi kuhusu kuwa salama mtandaoni, angalia habari kuhusu Mbinu za Kiteknolojia ‘Usalama katika sanduku‘.

Vifaa vilivyoshirikishwa

Kukaa salamu mkishirikisha vifaa na marafiki, wafanyikazi wenzako, wanafamilia au ukitumia kifaa kinachotumika na umma katika duka linalotoa huduma ya mtandao au maabara ya kompyuta, inaweza kuwa shida. Hakikisha kuwa hakuna mtu anyeweza angalia skrini yako. Futa historia yako ya kuvinjariukishamaliza na usisahau kutoka nje ya tovuti mitandao ya kijamii au akaunti unayoweza kuwa umetumia.

Kutumia VPNs

Ikiwa una wasiwasi kuhusu mtu yeyote kukufuatilia mtandaoni, unaweza tumia ‘VPN’ (Mtandao wa Kibinafsi wa Kweli). VPN inakusaidia kupata habari yako salama kuingia na kutoka katika kompyuta yako (usimbaji fiche) na inaficha lokesheni halisi uliko ili usiweze fuatiliwa, inakuruhusu kuvinjari bila kujulikana. Kuna chaguzi za programu zinapatikana kwa kupakuliwa mtandaoni.

Kufuta historia yako ya kuvinjari

Kufuta historia yako ya kuvinjari ni muhimu hasa wakati watu wengine wanatumia kifaa moja na wewe, lakini yafaa uifanye mara kwa mara ikiwa unatembelea tovuti inayoweza elezea watu kuhusu habari yako ya kibinafsi, kama mwelekeo wako wa kijinsia ama utambulisho wako wa kijinsia.

Nenosiri na pini

Nenosiri na nambari ya pini ni ya muhimu sana kwa usalama wako, hasa unaposhikisha vifaa. Hakikisha kuwa vifaa vyako vyote vina nenosiri rasibu ambazo zina herufi, nambari navihusishi maalum. Sentensi zinafanya vyema pia. Inavyokuwa ngumu zaid ndivyo inavyokuwa bora. Tumia nenosiri tofauti kwa kila kifaa na kila jukwaa/ barua pepe/ tovuti unayotumia. Hii itakurahisishia kudumisha faragha yako, hata kama kompyuta yako imedukuliwa au simu yako imeibiwa. Hakikisha kuwa umetoka nje ya akaunti unapomaliza kipindi chako. Unaweza pata programu za kidhibiti anuwai cha nenosiri mtandaoni ambayo itakurahisishia kuwa na pia kuhifadhi nenosiri ngumu.

Kutafuta nafasi

Kuwa mwangalifu kupata lokesheni ambayo unaweza fikia mtandao na programu katika faragha. Kimsingi hapa ni mahali ambapo hapana vikengeushi na ambapo wengine hawawezi tazama skrini yako bila wewe kujua. Fahamu kuwa matumizi ya programu za kusoma au vifaa visaidizi ambavyo vinatumia sauti vinaweza sababisha ukosefu wa faragha. Ikiwa utahitaji kuacha dodoso ili kufanya kitu kingine kabla hujamaliza, hakikisha kuwa umefunga skrini/kifaa ili mtu mwingine asiweze tazama unachofanyia kazi.