Rasilimali
Tafadhali kumbuka: Utafiti wa stadi ya SMILE hautoi huduma kwa watu. Ingawa tungependa kuwa na rasilimali ili kusaidia wanaohitaji huduma ya kiafya, afya ya kiakili au kukidhi mahitaji yao ya kila siku, hatuna uwezo wa kutoa huduma kupitia utafiti wa stadi hii.
Hata hivyo, ikiwa tutaskia huduma yoyote inayopeanwa kwa nchi yako inayoweza saidia wenye jinsia ya wachache ama ya walio wachache, tutafurahia kuchapisha habari hio kwenye tovuti hii. Tafadhali wasiliana nasi kutuambia rasilimali zinazopatikana na hazijanakiliwa hapa.
***unaona rasilimali yoyote iliyonakiliwa hapa ambayo si ya kirafiki au haisaidii wenye jinsia au kijinsia ya walio wachache? Tafadhali tujulishe kuihusu na tutaiondoa kutoka kwenye nakala!
Rasilimali Kenya
TRANS SUPPORT CBO KISUMU: Shirika ambalo lengo lake kuu ni kuunda kujulikana, kuimarisha fursa na kundeleza ustawi wa watu wa jinsia mbili tofauti, mtu aliyebadilisha jinsia na jinsia isiyo fuata jinsia za kawaida kwa watu wanaoishi mashinani mwa magharibi mwa Kenya.
Western Kenya LBQT Feminist Forum: Shirika ambalo lina umakini kwa kujenga harakati wa ufeministi kwa pande zote ambao utaezesha wanawake kushiriki kwa kufunya uamuzi, kujihusisha kwa uchumi na kijamii.
Kisumu Lesbians (KISLEB) Organization: Inalenga ushindi na utetezi wa haki za wanawake wasagaji, wenye jinsia mbili na wanawake ambao wanadadisi jinsia zao magharibi mwa Kenya.
Men Against AIDs Youth Group (MAAYGO): Inalenga afya iliyounganishwa, haki ya binadamu, utetezi wa sera na ustawi wa jumla wa GB-MSM walio katika eneo la Lake Victoria.
Nyanza Rift Valley and Western Network (NYARWEK): Mtandao wa LGBTQIA+ ambao unatetea haki ya wanachama kutoka magharibi mwa Kenya na Bonde la ufa.
Women Working with Women (3W): Inalenga kuhakikisha wanawake LBQ wanafurahia haki, uhuru na usawa.
SHINNERS CBO: Hili shirika lina lenga wanaume vijana kuanzia miaka 18 na zaidi wenye SRH. Kuimarisha uchumi, utetezi wa haki ya binandamu na taaluma ya kuingilia kati kwa maendeleo.
TINADA Youth Organization: Inalenga kwa kampeni za elimu kuhusu haki za afya ya kiakili iliounganishwa, kuimarisha mtoto na kijana, afya ya uzazi na kupunguza hatari ya maafa.
Keeping Alive Society’s Hope (KASH): Inalenga kwa huduma za afya zilizo unganishwa, haki za binadamu, kuezesha uchumi, utawala, utetezi wa sera na mashirika ya kimaendeleo na kumarisha mifumo.
Kisumu Male Sex Workers (KIMASWO): Shirika ambalo maono yake ni kukuza afya mzuri, haki ya binadamu, na kuezesha uchumi kwa wanaume wanaouza ngono magharibi mwa Kenya.
Gay and Lesbian Coalition of Kenya (GALCK): Ina umakini kwa kutambua, kukubalika na kutetea maslahi na haki ya mashirika ya LGBTI na wanachama wao ikijumuisha haki zao za kiafya.
Ishtar MSM: Shirika la kijamii Kenya lenye lengo la kupata haki kamili ya elimu ya afya ya ngono na ustawi wa kijamii kwa wanaume ambao wanafanya ngono na wanaume (MSM) Kenya.
Transgender Education and Advocacy: Shirika la Kenya ambalo lina lengo la kueneza ufahamu na kuunda mazingira yanayofaa kwa ustawi wa watu waliobadilisha jinsia na watu walio na jinsia tofauti Kenya.
Mpango wa Usalama