Maswali yanayoulizwa kila wakati
Ni nani anaweza kushiriki katika stadi ya SMILE?
Watu wanoweza kushiriki katika SMILE lazima:
- Wawe na umri wa miaka 18
- Uwe unaishi Brazil, Kenya au Vietnam kwa sasa
- Uwe na ufikiaji kwa tarakilishi au simu mahiri/kompyuta kibao na uwe na uwezo wa kumaliza dodoso la mtandaoni
- Uwe wa jinsia au kijinsia ya walio wachache. Kwa jinsia au kijinsia ya walio wachache tunamaanisha mtu yeyote ambaye:
- Anahisi mvutio wa kimapenzi au wa kingono kwa watu wengine wenye jinsia/ kijinsia iliyo sawa na yake au
- Anahisi mvutio wa kimapenzi au wa kingono kwa watu wa jinsia/ kijinsia zote: au
- Anajitambulisha kama asiyekuwa na hisia za kimapenzi- hujihisi kuwa na hisia za kingono ama kimapenzi kwa wengine
- Anajitambua kama jinsia iliyotofauti na jinsia au kijinsia aliyopewa wakati wa kuzaliwa au
- Anajitambulisha kama asiyefuata jinsia za kawaida- kumaanisha sio mwanamke au mwanaume au wakati mwingine ni kike amakiume
- Ni mwenye jinsia mbili tofauti au ana hali ya kuwa na jinsia mbili tofauti
Mwanafamilia/ Rafiki ni mwenye jinsia au kijinsia ya walio wachache. Naweza shiriki katika stadi la SMILE kwa niaba yao?
La, washiriki wote lazima wawe wanaweza kukamilisha dodoso kulingana na uzoefu wao wanaoupitia, na sio kujibu lkwa niaba ya mtu mwingine. Unakabirshwa kushiriki habari kuhusu stadi na mwanafamilia yako/ Rafiki na kuwahimiza kuchukua dodoso.
Dodoso linachukua muda gani?
Dodoso linaeza chukua kiasi cha dakika 15-20, kulingana na kasi utakayochukua kumalizia maswali, kuna pia fomu ya idhini ya mtandaoni , amabayo itachukua kadri ya dakika 10-15.
Nitapokea malipo kwa kumaliza dodoso?
La, hutapokea malipo kwa kukamilisha dodoso. Hii ni stadi ya kujitolea na tumaini kuwa watu watashiriki kwa hiari uzoefu wao kwetu, ili sauti zao na mahitaji yao yasikike.
Katika siku zijazo, washiriki wengine ambao washamlizia dodoso wanaeza kuwasliwa tena na wapatiwe nafasi ya kukamilisha dodoso linguine la kuongezea na/au kusaidia katika kuwaleta washiriki wengine. Ikiwa utatafutwa tena, unaeza kuwa unastahiki kupata malipo kidogo(ya $1-$5).
Sina ufikiaji wa tarakilishi na pia sina kifaa kilichowezeshwa kwenye tovuti kama simu mahiri/kompyuta kibao. Naweza kukamilisha dodoso la kibinafsi au nijaze dodoso hilo kupitia simu?
Pole, kwa wakati huu washiriki wote lazima watumie kifaa kilichowezeshwa kwenye tovuti kama vile tarakilishi,simu mahiri au kompyuta kibao ili kukamilisha dodoso hili. Katika siku zijazo, kunaweza kuwa na nafasi ya kushiriki katika stadi( kama kukamilisha mahojiano ya kibinafsi au kujiunga na kikundi cha kuzingatia); tutachapisha nafasi hizikwenye tovuti ya stadi kwa hivyo angalia tena kila wakati kwa matangazo ya aina hii.
Data yangu katika stadi itahifadhiwa kivipi?
Tunaelewa kuwa watu wengi wenye jinsia au kijinsia ya walio wacahache wanauzoefu wa ubaguzi, unyanyapaa na vurugu. Kwa sababu hii na kusaidia kulinda usiri wako, SMILE haitawahi ulizia jina lako.
Hata hivyo, kwa minajili ya kuwasiliana nawe kwa tafiti ya kufuatilia tutakuuliza nambari yako ya sim una anwani ya barua pepe: hii habari ya mawasiliano itahifadhiwa mbali na majibu yako ya dodoso. Majibu utakayopeana katika dodoso yatatumika tu kwa kusudi la utafiti na kwa njia ambayo haitaonyesha kuwa wewe ni nani. Habari yako ya mawasiliano itawekwa faragha na haitashirikiwa na yeyote nje ya mradi hu una habari yako ya mawasiliano haitaunganishwa moja kwa moja na majibu yako ya dodoso.
Wakati habari kutoka kwa hii stadi itakapowasilishwa katika mikutano ya kisayansi au itakapochapishwa katika majarida ya utafiti, vitambulisho vya washiriki havitafichuliwa. Huduma maalum itachukuliwa ili kulinda faragha ya washiriki ili watafiti wanaeza chambua data kutoka kwa dodoso hili: habari yoyote ya kibinafsi inayoweza tambulisha mtu yeyote itatolewa au kubadili kabla nakala za stadi zishirikiwe na watafiti wengine.
Mbona nishiriki katika utafiti huu, ikiwa stadi ya SMILE hainitolei huduma yoyote?
Swali nzuri! Hii ndio sababu ya sisi kutarajia kuwa utakuwa mkarimu sana na kutupea muda wako wa kutosha ili kuchukua muda kufanya dodoso na kushiriki uzoefu wako nasi.
Hadi sasa, tafiti nyingi zinazohusisha wenye jinsia/ kijinsia ya walio wachache imefanywa katika nchi zenye pato za juu kama vile U.S au nchi za Western Europe. Stadi chache sana zimefanywa katika nchi zingine kama vile Brazil,Kenya na Vietnam. Hapo kale, tafiti nyingi zinazojumuisha wenye jinsia/kijinsia ya walio wachache zilikuwa:
- kiwango kidogo (inayohusisha nchi moja au washiriki mia chache); au
- zinazingati HIV au tabia hatari za HIV, au hali zingine za kiafya; au
zinazingatia idadi maalum ya watu(kama vile wanaume wanaoshiriki ngono na wanaume au wanawake walio na jinsia tofauti na waliozaliwa nayo) huku wakitenga makundi mengine.
Kaika stadi ya SMILE, tunataka kujifunza kuhusu afta na hali ya kiakili na hali ya kihisia na uzoefu wa Maisha wa watu wote wenye jinsia au kijinsia ya walio wachache (juu ya 10,000) kutoka nchi tatu tofauti. Lengo letu ni kukusanya data ili kuelewa jinsi ambavyo sera,mipango na huduma zinawezaundwa au kutengenezwa ili kusaidia kutoa msaada kwa wenye jinsia au kijinsia ya walio wachache.
Ukishiriki kwenye stadi, utakuwa na nafasi ya kuwakilisha wanachama ya jinsia au kijinsia ya walio wachache kwa kushiriki uzoefu wako wa kibinafsi wa afya ya kiakili ambayo itatumika kuamua mahitaji, vizuizi na mapendeleo sahihi vya matibabu ya afya ya kiakili ambayo itatumika baadaye kutengeneza sera na miongozo ya afya ya kiakili ya wenye jinsia au kijinsia ya walio wachache na kushawishi programu ya afya ya kiakili kwa jinsia au kijinsia ya walio wachache nchini Kenya.
Ni jinsi gani matokeo ya stadi yatawasilishwa?
Matokeo ya stadi yataanza kupatikana wakati washiriki wote wamesajiliwa na kukamilisha dodoso(mwisho wa 2022 kwa karibu). Muhtasari wa data ya dodoso itachapishwa hapa katika tovuti ya SMILE, pamoja na viungo vya uchapishaji wa stadi.
Watafiti wa stadi wamejitolea kuchapisha kwa majarida ya ufikiaji wazi pekee- hiyo ni kumaanisha, majarida ambayo yeyote(washiriki, watafiti, waundaji sera na wanaumma) wanaeza fikia kwa urahisi. Machapisho kamili ya maandishi yatapatikana pekee kwa Kiingereza: hata hivyo, tutahakikisha kuwa muhtasari wa matokeo yanapatikana katika Portuguese, Kiswahili na Vietnamese.
Wanachama wa timu ya watafiti (FIOCRUZ nchini Brazil, Ace Africa nchini Kenya na LIFE Centre nchini Vietnam) yatafanya kazi ili kusambaza na kuwasilisha matukio kw bodi za ushauri za jamii na wadau wa ndani wakati zitapatikana.
Usaidizi! Nilianza kuchukuwa dodoso lakini kitu kikafanyika na ukurasa wa wavuti ukajifunga / ukaganda /sikumalizia dodoso. Nifanye aje?
Tafadhali angalia ukurasa wetu”utatuzi wa shida” maswala ya kawaida ya dodoso na maazimio.
Naweza wasiliana na nani na haya maswali?
Ikiwa una maswali yoyote kuhusu utafiti wa stadi au unahitaji usaidizi na dodoso, tafadhali angalia ukurasa”wasiliana nasi” kwa habari ya mawasiliano.