Ushiriki wa Dodoso la SMILE

Ni kipi ambacho nastahili kufanya ili kushiriki?

  1. Hakikisha kuwa unastahiki:
    • Lazima uwe na umri wa miaka 18 au zaidi
    • Lazima uwe unaishi Brazil, Kenya au Vietnam kwa sasa
    • Lazima uwe na anwani ya barua pepe ambayo ni wewe pekee unayeitumia
    • Lazima uwe na nambari yako kibinafsi ya simu
    • Lazima uwe na ufikiaji wa mtandao(nyumbani ama kwingineko)
  2.  Bonyeza kidude cha “chukua dodoso” pale chini ya ukurasa huu. Hii itakupeleka kwenye tovuti la dodoso, ambapo URL inaanza na https://duke.qualtrics.com/…
  3. Soma fomu ya idhini ya mtandaoni kwa makini. Ikiwa una swali lolote, tafadhali wasiliana na timu ya stadi ili kuwezesha kujibu kabla ya kuendelea kupita hapa.
  4. Kisha ingiza habari yako ya mawasiliano na ujibu maswali machache ya haraka kujihusu. Hii habari itawekwa kando na habari yoyote ile utakayopeana kupita hapa. Itatumika tu ikiwa tutahitaji kuwasiliana nawe ili ushiriki Zaidi.
  5. Hatimaye, malizia dodoso. Hii itakuchukuwa kama [dakika 15-20] ikiwa itafanywa yote mara moja,ingawa inawezekana kuacha dodoso na uirejelee baadaye.  Ikiwa una maswali yoyote kuhusu dodoso lenyewe au changamoto unayopitia ukiifanya, tafadhali rejelea utatuzi wa shida na ukurasa ya maswali yanayoulizwa kila wakati katika tovuti hii. Tafadhali kumbuka, hutapokea malipo yoyote kwa kuchukua dodoso hili.

 

Asante kwa kuzingatia na kuonyesha hamu katika utafiti wetu!